Mchangani

KAUZU WATINGA NUSU FAINALI, YAILAZA KIDABA DAKIKA ZA MWISHO

Mashabiki wa Kauzu wakati wakiingia uwanjani hii leo katika kipindi cha pili cha mchezo
Timu ya soko la Tandika Kauzu FC wamefanikiwa kutings hatua ya nusu fainali ya michuano ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndando cup inayoendelea katika uwanja wa Bandari jijini Dar es salaam.

Leo Kauzu walikuwa wanawania nafasi hiyo ya kutinga nusu fainali dhidi ya Kidaba One na kushuhudia Kauzu wakifainkiwakuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kauzu iliwabidi wangoje mpaka dakika ya 90 kuandika goli hilo pekee ambalo lilifungwa na Rashid Roshwa.

Katika mchezo huo Kidaba ndio waliotengeneza nafasi nyingi za kufunga na katika kipindi cha pili ndio waliotawala mchezo huku katika kipindi cha kwanza utawala wa mchezo ukiwa sawa kwa kila upande.

Matokeo hayo ya ushindi yanaifanya Kauzu kupambana na Misosi FC ya Tandale katika nusu fainali ya Pili huku Makumba FC wakipambana na Temek Market katika nusu fainali ya kwanza

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.