Mchangani

KISIGA AIVUA UBINGWA TIMU YAKE, ATINGA NUSU

Mtoto shabiki wa timu ya Faru Jeuri akiwa amevaa kimasai ndani ya uwanja wa Bandari Temeke
Kiungo wazamani wa Simba SC, Azam FC, SC Villa na Mtibwa Sugar Shaban Kisiga leo ameiongoza Temeke Market kuiondosha timu yake ya mtaa  na timu aliyotwaa nao ubingwa wa kombe la Sports Extra Ndondo Cup mwaka jana Faru Jeuri ya vingunguti jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa leo wa kwanza wa robo fainali ulishuhudia Temeke Market ikiibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya Faru Jeuri na kuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Goli pekee la Faru Jeuri lilifungwa na Ramadhan Madebe katika kipindi cha kwanza cha mchezo na kuipeleka timu yake hatua ya nusu fainali.

A

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.