Mchangani

MAKUMBA FC WAFANIKIWA KUTINGA ROBO FAINALI, WAITOSHA KEKO KWA MATUTA

Makumba FC wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup inayodhaminiwa na kituo cha Forplan Clinic, Azam TV, Mwanaspoti na Startimes baada ya kuwafunga kwa mikwaju ya penati Keko Furniture.

Keko Furniture walikuwa wa mwanzo kupata goli katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Alex Zegege katika dakika 24 kwa shuti kali goli lililo dumu kwa takribani dakika 76 kwani Makumba FC walisawazisha goli hilo katika dakika ya 90 kupitia kwa Ally Mohammed 'Gaucho' na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Katika mikwaju ya penati, Makumba FC walifanikiwa kufunga penati 7 kati ya nane, wakati Keko Funiture wakipata penati 6 kati ya 8 walizopiga, na Makumba FC kufanikiwa kuwa timu ya nne kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.