Mchangani

MAKUMBA WAIFUATA TEMEKE NUSU FAINALI

Makumba FC wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya sports xtra ndondo cup inayodhaminiwa na Dr Mwaka, Azam TV na Mwanaspoti, baada ya kuifunga Tabata United kwa mikwaju ya penati 3-1.

Katika mchezo wa leo wa pili wa robo fainali. ulishuhudia Tabata United wakicheza dakika 45 za kipindi cha pili wakiwa pungufu baada ya dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza mchezaji wao kupewa kadi nyekundu.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za wenzake, huku Makumba FC wakipoteza nafasi nyingi za kufunga ukilinganisha na Tabata united.

Kipindi cha pili kilianza kwa Tabata united kuandika goli la kwanza kupitia kwa Gerard Mdimu katika dakika ya 46 kabla ya Mkumba FC kusawazisha katika dakika ya 89 kupitia kwa Mustafa Khamisi na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Makumba FC walifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata mikwaju mitatu ya penati kati ya minne huku Tabata wakiapata mmoja kati ya mikwaju mitatu walio piga.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.