Mchangani

MISOSI WATINGA NUSU KWA MIKWAJU YA PENAT

Shabiki akifuatilia mchezo wa robo fainali ya Sports Xtra Ndondo Cup
Robo fainali ya tatu ya Dr Mwaka Sports Xtra Ndondo cup, imechezwa leo katika uwanja wa Bandari Tandika jijini Dar es salaam na kushuhudia Misosi ya Tandandale ikifanikiwa kutinga hatua ya nsu fainali.

Misosi FC leo walikuwa wanacheza na Goms United na mpaka dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyokuwa imefunga goli na Misosi kuiondosha Goms kwa mikwaju ya penati.

Misosi FC wamepata penati zote 4 walizopiga huku Goms wakpata penati 2 kati ya penati 4 walizopiga.

Robo Fainali ya Mwisho inatarajia kuchezwa siku ya jumapili kati ya Kidaba One na Kauzu katika uwanja wa Bandari.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.