Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys hii leo ameibuka na ushindi wa goli 6-0 mbele ya mashabiki wa Shelsheli katika mchezo wa marejeano kusaka tiketi ya kushiriki mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.
Katika mchezo wa leo uliochezwa nchini Shelisheli Serengeti Boys walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0, ambapo goli la kwanza lilifungwa katika dakika ya 9 kupitia Ibrahim Abdallah aliyemalizia mpira uliotemwa na kipa wa Shelisheli kufuatia shuti la Asad Juma.
Asad Juma aliiandika Serengeti boys goli la tau katika dakika ya 50 kabla ya Issa Mwakamba kufunga goli la 4 katika dakika ya 61.
Saad Juma aliiandikia Serengeti boys goli la tano katika dakika 70 kabla ya kupata goli la 6 na kupelekea mchezo kumalizika kwa Serengeti boys kuibuka na ushindi wa goli 6-0.
Kwa matokeo hayo ya leo Serengeti boys wamewatoa Shelisheli kwa matokeo ya jumla ya goli 9-0, na sasa watakutana na Sauzi Afrika katika hatua inayofuata ya kusaka tiketi ya kwenda Madagascar mwakani
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment