Mchangani

TABATA UNITED WAKIWA PUNGUFU WATINGA ROBO FAINALI

Wachezaji wa  Tabata United wakimpongeza mchezaji mwenzao Gerald Mdamu baada ya kufunga bao la kuongoza katika mchezo wa leo dhidi ya Kiluvya United 
Tabata United wakiwa pungufu wamefanikiwa kuwatoa Kiluvya united katika michuano ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndondo Cup na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuanpo hiyo inayodhaminiwa na gazeti la Mwanaspoti, Stars Times, Azam TV, Forplan.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa umepoa kulinganisha na michezo miwili iliyopita ya hatua hiyo ya mtoano, mchezaji wa Tabata United alizawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 20, na kupeleka Tabata united kumaliza wakiwa pungufu.

Tabata United waliandika goli lao pekee katika mchezo wa leo kupitia kwa Gerald Mdamu katika dakika ya 40 ya mchezo, goli lililodumu dakika zote tisini za mchezo.

Kwa ushindi hu Tabata united wanaungana na Temeke Market na Faru Jeuri kutinga hatua ya robo fainali huku wakiondoka uwanjnai na kitita cha shilingi laki tatu, huku Kiluvya united wakiondoka na shilini laki mbili na kutolewa katiaka michuano hiyo.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.