Mchangani

TEMEKE MARKET NDIO MABINGWA WA NDONDO


Mabingwa wa Sports Xtra Ndondo Cup 2016, Temeke Market
FC Kauzu ya Tandika sokoni jijini Dar es salaam imepoteza fainali ya pili mfululizo ya michuano ya Sports Xtra Ndondo cup, baada ya leo kupotza mbele ya Temeke Market na kupelekea Temeke Market kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Katika mchezo wa leo ulishudia magoli manne yakifungwa katika kipindi cha kwanza, ambapo Temeke Market wakifunga magoli 3, na Kauzu wakipata goli 1.

Magoli ya Temeke Market yalifungwa na Madebe Ramadhan katika dakika ya 6, Shaban Kisiga dakika ya 31 na Adam Kingwande katika dakika ya 41.

Goli la FC Kauzu likifungwa na Rashid Gumbo na kupelekea mchezo kumalzika kwa FC kauzu kufungwa goli 3-1 na Temeke Market.

Nchezaji bora wa michuano ya mwaka huu alikuwa kiungo ambae ametwa taji hilo mara mbili mfululizo Shaban Kisiga, ambapo msimu uliopita alitwaa taji hilo akiwa na Faru Jeuri na mwaka huu kuchukuwa akiwa na Temeke Market.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.