Mchangani

TEMEKE MARKET WATANGULIA FAINALI, WAICHAPA MAKUMBA KWA PENATI

Temek Market wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndondo Cup baada ya leo kuitoa kwa mikwaju ya penati Makumba FC katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa leo katika uwanja wa Bandadri jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ulishuhudia dakika 90 zikimalizika kwa sare ya bila kufungana na katika hatua ya penati Temeke Market walishinda penati tatu kati ya nne huku Makumba FC wakishinda penati 1 kati ya nne walizopiga.

Dakika moja kabla ya mchezo kumalizika Temeke Market walifanikiwa kutia mpira katika nyavu za Makumba FC, lakini mwamuzi wa mchezo huo alilikataa goli hilo, kitendo kilichopelekea Mtafaruku kwa mashabiki wa liofika hapo uwanjani na jeshi la poilisi wakishirikiana na baadhi ya mashibiki walifanikiwa kuzuia mtafaruku huo na mikwaju ya penati ikapigwa.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.