CAF

MEDEAMA WASITISHA SAFARI YA YANGA CAF, WAICHAPA MAZEMBE 3-2

Matumaini ya mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya shirikisho (CAF Confederation Cup) yamepotea baada ya leo Medeama ya Ghana kuibuka na ushindi wa goli 3-2, walipo wakaribisha TP Mazembe.

Medeam sasa wanahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mo Bejaia ili itinge nusu fainali wakati TP Mazembe wao teayari wameshatinga nusu fainali.

Ushindi wa leo wa Medeama unaifanya ufikishe poiti nane ambazo yanga sc hawawezi kuzifikia hata kama wakiwafunga TP Mazembe katika mchezo wao wa mwisho utakao chezwa  agusti 23 mwaka huu.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.