simba

MGOSI AAGWA KWA SARE YA 1-1


Mchezo wa kumuaga naodha wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi umemalizika kwa sare ya goli 1-1, mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Simba SC leo wamecheza mchezo wa kirafiki na URA ya Uganda na mpaka dakika 45 za mwanzo zinamalizika ubao wa matokeo ulikuwaunasomeka kwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo huo uliojaa ufundi mwingi huku kila timu ikijaribu kutawala eneo la kati ya uwanja kwa kupokezana, na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambapo kila mmoja akitumia nafasi moja.

Walikuwa URA wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Nkugwa Elikana katika dakika 20 ya mchezo kabla ya Jonas Mkude kuisawaizishia Simba SC katika dakika ya 32 ya mchezo na kupeleka mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo huo maalum ambao ulitumika kumuaga nahodha wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi aliyetangaza kustaafu kucheza mpira na sasa atakuwa meneja wa timu hiyo, Mgosi alicheza kwa dakika 3 za mwanzo za mchezo na kumpisha Jamal Mnyate.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.