CAF

SERENGETI BOYS WAIDUWAZA SOUTH AFRIKA, WAWALAZIMISHA SARE


Timu ya taifa ya soka chini ya miaka 17 Serengeti Boys, wamewalazimisha sare ya goli 1-1 kwa vijana wenzao wa South Afrika katika mchezo wakusaka nafasi ya kucheza mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 mwakani nchini Madagascar.

Katika mchezo huo wa leo uliochezwa nchini Afrika kusini , ulishuhudia dakika 45 za mwanzo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Katika kiipindi cha pili Afrika kusini walifanikiwa kupata goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Luka de Roux katika dakika ya 65, kabla ya Serengeti Boys kusawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Ali Mtengi katika dakika ya 75, na kupeleka mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Matokeo ya mchezo huo unawaweka katika mazingira mepesi Serengeti boys katika mchezo wa marejeano utakoa chezwa agusti 21 katika uwanja wa Azam Complex, ambapo watahitaji sare ya bila kufungana ama kushinda kwa idadi yoyote ya magoli. na endapo watatoka sare ya goli 2-2 na zaidi Sernegit boys watashindwa kusonga mbele.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.