CAF

TP MAZEMBE WAICHAPA YANGA GOLI 3, VICENT AKIPEWA NYEKUNDU

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wamemaliza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika wakiwa wa mwisho kwenye kundi A, huku TP Mazembe wakifanikiwa kumaliza kama vinara wa kundi hilo baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

Katika mchezo huo wa leo uliochezwa katika uwanja wa TP Mazembe, Yanga SC walijikuta wakimaliza wakiwa pungufu baada a Andrew Vicebt kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika a 30 ya mchezo.

TP Mazembe waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 28 kupitia kwa Jonathan Bolingi, goli hilo lilidumu kipindi chote cha kwanza.

Katika Kipindi cha pili TP Mazembe walifanikiwa kuandika goli la pili Rainford Kalaba katika dakika a 54 kabla ya kufanya hivyo tena katika dakika ya 58.

Goli pekee la Yanga hii leo lilifungwa na Amisi Tambwe katika dakika ya 74 na kupelekea mchezo kumalzika kwa TP Mazembe kutinga nusu fainali wakiwa vinara wa kundi A.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.