Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wameweka rikodi katika michuano ya CAF katika hatua ya makundi baada ya kupata ushindi wa kwanza katika historia ya timu hiyo katika hatua hiyo ya michuano ya CAF.
Yanga SC leo wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mo Bejaia katika mchezo watano wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika, mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa.
Katika mchezo wa leo Yanga SC walipoteza nafasi kadhaa ya kupata magoli ya kutosha kupitia kwa Obrey Chirwa na Saimon Msuva, na Mo Bejaia nao hawakuwa nyuma katika kupoteza nafasi walizo tengeneza.
Katika mchezo wa leo goli pekee la Yanga SC lilipatikana katika dakika ya 3 kupitia kwa Amisi Tambwe na goli hilo kudumu kwa dakika zote 90.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga SC kuwa na matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya vilabu barani Afrika.
Kikosi Cha Yanga leo: Deo Munish, Juma Abdul/Said Juma, Mwinyi Hajji, Vicent Bosue, Andrew Vicent/Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Saimon Msuva, Thaban Kamusoko, Amisi Tambwe, Chirwa, Deusi Kaseke/Juma Mahadhi

0 comments:
Post a Comment