simba

SIMBA WAENDELEA KUTAKATA, WAILAZA 2 KAGERA

Vinara wa ligi kuu ya vodacom Simba SC wameendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu baada ya kuendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuwafunga Kagera Sugar goli 2-0, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Simba SC waliandika goli katika kila kipindi, goli la kwanza wakifunga kupitia kwa Mzamiru Yassini katika dakika ya 41 ya mchezo.

Goli la pill hii Leo la simba sc limefungwa na Ramadhan Shiiza Kichuya kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili na kupelekea Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Katika uwanja wa CCM Kambarage hii Leo Stand united wameendelea kutopoteza mchezo baada ya kwenda sare ya goli 1-1 na African Lyon, huku JKT Ruvu wakienda safe ya goli 1-1 na Mwadui FC

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.