simba

SIMBA SC WAREJEA KILELENI, AZAM WAKIAMBULIA SARE

Simba SC wamefanikiwa kurejea kileleni hii leo baada ya kuifunga Ndanda FC magoli 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Katika mchezo huo iliwabidi Simba SC kungoja mpaka kipindi cha pili ambapo walifanikiwa kupata magoli hayo mawili kupitia kwa Mohammed Ibrahim na Mzamiru Yassin.

Ushindi huo wa goli 2-0 unaifanya Simba ikae kileleni kwa kufikisha pointi 38 wakiwa mbele ya yanga kwa pointi mbili.


Katika hatua nyingine Azam FC wameshindwa kutamba mbele ya African lyon na hatimae kuambulia sare ya bila kufungnana, wakati Mbao FC wakiifunga Stand united kwa goli 1-0 katika uwanja wa CCM Kirumba.



MATOKEO VPL LEO

TANZANIA PRISONS 1-0 MAJIMAJI
MBAO FC 1-0 STAND UNITED
NDANDA FC 0-2 SIMBA SC
AFRICAN LYON 0-0 AZAM FC


MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM

RnTimuPWDLFAGdPts
1SIMBA SC1612222862238
2YANGA1611323482636
3Azam FC167542314926
4KAGERA SUGAR167451616025
5MTIBWA SUGAR166642019124
6STAND UNITED165741513222
7T. PRISONS165741010022
8Ruvu Shooting164841517-220
9MBEYA CITY165561315-220
10NDANDA FC165471318-519
11Mbao FC165381620-418
12African Lyon164661015-518
13MWADUI FC164481321-816
14MAJIMAJI FC1651101224-1216
15JKT RUVU16277615-913
16TOTO AFRICANS163310918-912

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.