VPL

NGOMA AIOKOA YANGA MBELE YA MAJIMAJI


Goli la Donald Ngoma limeifanya yanga SC kuambulia Sare katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa hii leo katika uwanja wa Majimaji mjini Songea dhidi ya Majimaji FC.

Katika mchezo huo wa tatu kwa kila timu ulishuhudi timu hizo zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana huku kila timu ikiajribu kusaka goli la kuongoza.

Katika kipindi cha pili Majimaji FC ndio walikuwa wa mwanzo kuona nyavu za yanga kupitia kwa Peter Mapunda katika dakika ya 54 kabla ya Donald Ngoma kuisawazishia yanga kwa kichwa katika dakika ya 79 akimalizia krosi ya Chirwa.

Matokeo ya mchezo huo ambao Majimaji waliingia uwanjani kwa mlango wa nyuma unaifanya yanga kufikisha pointi 5 wakiwa nyuma kwa pointi 4 na vinara Mtibwa Sugar.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.