vilabu

PHIRI AACHANA NA MBEYA CITY

Klabu ya Mbeya City FC leo tarehe 13.09.2017 imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha Mkuu wake Kinnah F. Phiri.

Kikao cha leo ulikuwa ni muendelezo wa vikao kadhaa baina ya pande hizi mbili toka mwezi julai mwaka huu. Baada ya majadiliano marefu pande zote mbili zimekubaliana kutoendelea na makubaliano yao ya hapo awali.

Sababu kubwa ni matokeo mabaya ya timu ya msimu uliopita 2016/2017 ambayo yameipunguzia klabu uwezo mkubwa wa kuhimili mahitaji yake ya msingi baada ya wadhamini waliotarajia kuingia kushindikana na wadhamini waliopo kupunguza kiwango cha udhamini wao kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha.
Klabu itatangaza kocha mkuu baada ya muda mfupi ujao ila kwa sasa timu itabaki chini ya usimamizi wa kocha msaidizi Mohamed Kijuso.
Klabu inapenda kumshukuru Kocha Phiri kwa mchango wake muhimu katika timu yetu, itaendelea kuuthamini na kuukumbuka na inaamini Kocha Phiri ataendelea kuwa msaada katika maendeleo ya timu yetu kwani amekuwa sehemu ya familia yetu.

Wasalaam,
Shah Mjanja
Afisa Habari
0623 154077

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.