simba

SIMBA SC YAREJEE KILELENI, YAICHAPA STAND MBILI

Mabingwa wa kombe LA shirikisho la soka nchini, Simba SC wamefanikiwa kurejea kileleni leo baada ya kuifunga Stand united goli 2-1 na kufikisha pointi 11 sawa na Mtibwa sugar na Azam FC, wakiwa na idadi kubwa ya magoli ya kufunga.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Simba SC walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, goli lililofungwa na Ramadhani Shiiza Kichuya katika dakika ya 17.

Simba SC waliandika goli la pili katika dakika ya 47 kupitia kwa Laudit Mavugo, kabla y Stand united kujipatia goli lao pekee hii leo kupitia kwa Mutasa Munashe katika dakika ya 51 na kupelekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kushinda goli 2-1.

Ligi kuu ya vodacom inatarajia kuendelea baada ya wiki mbili ambapo wiki ijayo ni maalumu kwa michezo ya timu za Taifa.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.