VPL

KAGERA WAICHAPA MAJIMAJI, MCHEZO WA PRISONS KUHITIMISJWA KESHO

Mabingwa wa zamani wa kombe la Tusker, Kagera sugar leo wamefanikiwa kuvuna pointi tatu katika uwanja wake wanyumbani wa kaitaba baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mbele ya Majimaji FC.


Kagera sugar walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Edward Christopher katika dakika za mwisho wa kipindi cha kwanza na kuplekea mchezo kwenda mapumziko Kagera sugar wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika Kipindi cha pili Majimaji FC walirejee kwa nguvu na kufanikiwa kupata goli la kusawazusha kupitia kwa Jerson Tegete kabla ya Japhet Makarai kuifungia Kagera Sugar goli la pili na la ushindi.


Ushindi huo wa goli 2-1 unaifanya Kagera sugar kufikisha pointi 18 sawa na Njombe Mji na Ndanda FC huku wakiiacha Majimaji FC ikibuluza mkia wakiwa na pointi zao 15.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom ulio wakutanisha Tanzania Prisons na Mbao umeshindwa kumalizika kutoka na mvua zinazoendelea kunywesha jijini Mbeya kupeleka uwanja kujaa maji.

Mchezo huo uliokuwa unachezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya mpaka unasimama Prisons walikuwa mbele kwa goli 1-0, goli lililofungwa na Muhamed Rashid katika dakika ya 11 ya mchezo.

Mchezo huo utaitimishwa kesho saa nne asubuhi kwa kuchezwa dakika 40 zilizo kuwa zimesalia baada ya mwamuzi kuvunja mchezo katika dakika ya 50 kutokana na uwanja kujaa maji.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.