CAF

KOCHA WA ROLLERS TUPO TEYARI


Kocha wa Township Rollers ya Botswana Nikola Kavazonic amesema kuwa watazama michezo minne ya yanga ambayo anaimani itampa kile alichokuja kukipata hapa nchini Tanzania apo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Kavazovic amesema kuwa analijua vilivyo soka la Afrika, na anekuwa akilifuatilia vizuri, na timu yake iko vizuri kwa mapambano hapo kesho katika mchezo wa klabu bingwa Afrika.


Township Rollers inacheza na yanga kesho ikitokea kuitoka El-merrekh katika mchezo wa raundi iliyo pita.


Wakati huo huo katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amesema kuwa mchezo wa kesho ni mchezo mkubwa na ushindani na mshindi anaingia moja kwa moja hatua ya makundi ambapo ndipo kwenye hela.

"Hii ni mechi kubwa na ya ushindani, mshindi anakwenda kwenye hatua za makundi. Kama mnavyofahamu hatua ya makundi wanasema ni ‘money zone’ ni eneo ambalo timu inapoingia kuna kuwa hakuna figisu za kutokuwa na pesa.”

“Kufuzu hatua hii kutaleta mafanikio kwenye klabu kwa hiyo kila timu inapambana kufika pale ili kujaribu kupunguza japo gharama za maandalizi kwa sababu mashindano haya yanatumia gharama kubwa sana. Sisi tuna nia ya dhati kabisa kufanya vizuri na tumejipanga.” alisema Mkwasa

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.