VPL

LIPULI WAENDELEA KUKWEPA KUSHUKA, WAICHAPA NDANDA

Magoli mawili ya Adam Salamba imeifanya Lipuli kuendelea kukimbia hatari ya lushuka daraja baada ya kufikisha pointi 23 kufuatia ushindi walioupata leo mbele ya Ndanda FC iliyopo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Samora mkoani Iringa umeshuhudia Lipuli wakiandika goli la kwanza kupitia kwa Adam Salamba katika dakika ya 19.

Ndanda FC walijibu mapigo na ndani ya dakika mbili walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa Nassoro Kapama ikiwa ni dakika ya 21 na kupelekea mchezo kwenda mapimziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Katika dakika ya 64 Adam Salamba aliifungia Lipuli goli la pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa Lipuli kushinda goli 2-1.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.