VPL

MTIBWA SUGAR WACHAPWA, MAJIMAJI WAKITOA SARE

Wakata miwa wa Manungu Mtibwa Sugar leo wamekubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Tanzania Prisons wakati Majimaji FC inayo buluza mkia wakiambulia sare ya bila kufungana toka kwa Lipuli katika mwendelezo wa ligi kuu yavodacom Tanzania Bara.

Katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, Tanzania Prisons hii leo walikuwa wenyeji wa Mtibwa sugar ambapo hadi wanakwenda mapumziko matokeo yalikuwa yanasomeka goli 1-1.

Mtibwa Sugar ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Stamili Mbonde katika dakika ya 32, wakati Tanzania Prisons wakisawazisha goli hilo katika dakika za mwisho wa kipindi cha kwanza kupitia kwa Salum kimenya.

Katika kipindi cha pili Prisons walifanikiwa kufunga goli la pili katika dakika ya 49 kupitia kwa Salum Kimenya na kuipa Prisons ushindi wa goli 2-1.

MATOKEO MENGINE YA MICHEZO YA LEO VPL

MAJIMAJI FC 0-0 LIPULI FC
SINGIDA UNITED 0-0 NDANDA FC
RUVU SHOOTING 2-2 MBEYA CITY

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.