VPL

PRISONS WAKAMILISHA 40 VYEMA, MBEYA CITY WABANWA SOKOINE


Tanzania Prisons wamefanikiwa kulinda goli lao walilopata hapo jana katika mchezo uliochezwa kwa dakika 50 na leo hii kuhitimisha dakika 40 zilizo kuwa zimesalia.

Hapo jana Tanzania Prisons walikuwa weneyeji wa Mbao FC mchezo uliochezwa kwa dakika 50 kabla ya kusimamishwa kutokana na uwanja kujaa maji na hii leo u,ehitimishwa kwa kutoshuhudia goli lolote lile katika dakika hizo 40.

Kutokana na hivyo Tanzania Prisons wanaibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililo fyngwa hapo jana katika dakika ya 11 na Mohammed Rashid kwa mkwaju wa penati.

Wakati Tanzania Prisons wakishangilia ushind huo katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, jirani zao Mbeya City wametoka sare ya bila kufungana na Mwadui FC katika mchezo ulioanza saa nane mchana katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.