VPL

SINGIDA WALAZIMISHA SARE, MBAO WAKICHAPWA SOKOINE

Goli la Kennedy Juma katika dakika ya 74 limeiokoa Singida United kutoka kupoteza mchezo mbele ya Ruvu shooting katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Namfua  mkoani Singida.

Katika mchezo huo, Ruvu shooting waliandika goli lao la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa Issa Kanduru na kupelekea mchezo kwenda mapumzikoRuvu shooting wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Singida United walikuja kusawazisha goli hilo katika dakika ya 74 kupitita kwa Kennedy na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliochezwa hii leo umeshuhundi Mbao FC wakiendelea kudidimia baada ya leo kukubali kipigo cha goli 2-1 toka kwa Mbeya City mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Magoli ya Mbeya city katika mchezo huo yalifungwa na John Kabanda dakika ya 0 na Eliud Ambokile dakika ya 48 kwa mkwaju wa penati huku la Mbao FC likifungwa na Herbert Lukindo katika dakika ya 63.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.