VPL

YANGA KUJIULIZA KWA KAGERA SUGAR KESHO


Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga SC kesho watashuka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuikabili Kagera Sugar katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara inayo dhaminiwa na Vodacom.

Yanga SC katika mchezo huo wa kesho anaitaji ushindi ili kuendelea kuifukuzia Simba SC katika mbio za ubingwa wa ligi.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Habari wa Yanga Dismas Teni amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo wa kesho yako teyari na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.

"Kwa ujumla matayarisho ya mchezo wa kesho yamekamilika, ni mechi ya nyumbani na tunahitaji kupata matokeo, nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kuisapoti timu, shabiki wa kweli ni yule anayekuja uwanjani kuitazama timu yake" amesema Teni.

Endapo Yanga SC wakishinda kesho atakuwa amepunguza wigo wa pointi baina yake na Simba SC kutoka pointi 6 hadi kufikia pointi 3.

Kagera sugar katika msimu huu wamekuwa na msimu mbaya kwani kwa sasa yupo katika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 18 wakiwa wamecheza michezo 20.

Endapo Kagera Sugar akishinda kesho atajisogeza mpaka katika nafasi 11 akiwa na point 21.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.