aamsuni
MECHI ya watani wa jadi, Yanga na Simba uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi umeingiza sh. 243 ,017 ,000 kutokana na watazamaji 46 ,539 waliokata tiketi kuishuhudia. Kutokana na mapato hayo kila timu imepata sh. 51 ,194 ,793 baada ya makato mbalimbali ya gharama za mchezo kukatwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba mapato hayo yametokana na kuuzwa kwa tiketi zote za viti vya kijani 19 ,648 na bluu 17 ,045. "Maeneo ambayo tiketi hazikuuzwa zote ni viti rangi ya machungwa, Viti Maalum A (VIP A), VIP B na VIP C ambapo kati ya tiketi 748 sawa na viti 748 , tiketi 309 ndizo zilizouzwa, hivyo ukichanganya mapato yote hayo unapata fedha hizo," ilieleza taarifa hivyo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya kuondoa gharama za mchezo na mgao wa uwanja, Kodi ya Ongezeko la Mapato (VAT), Chama cha Soka cha Mkoa (DRFA), TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) huku klabu zikipata sh. 51 ,194 ,793.
0 comments:
Post a Comment