Mchangani

Issa kuwaongoza wamasai Sudan

Issa katika moja ya mechi ya 
wanafunzi wa Tanzania
Wanafunzi wa Tanzania wanao soma katika chuo cha Internationa University of Africa (IUA) kilichopo Sudan, kesho asubuhi watakuwa na mpambano kati ya wale wanao kimbilia kutimiza mwaka 'wamasai' na wale wakongwe.
Mchezo huo utakao chezwa katika uwanja mdogo iliyopo Markaz chuoni hapo, ni maalum kwa ajili ya kuunda kikosi cha Tanzania kitakacho kuwa kinawakilisha wa Tanzania katika mashindano mbalimbali ya hapo chuoni chini ya katibu wa michezo na utamaduni, Mbarouk.

Tanzania ambayo ilitolewa katika hatua ya makundi katika mashindano ya Africa mashariki na kati wanadhamira ya kurudisha makali ambayo yalikwisha aanza kupotea.

Kikosi cha masai kitakacho ongozwa na mshambuliaji mahiri wa Tanzania kwa sasa Amir Issa akisaidiwa nyota wengine wanaunda kikosi cha Tanzania, Yusuph, Adam pamoja na kipa aliyeshindwa kutamba Abdallah Hamdun 'aboodmsuni'.

Wakati wakongwe wakiwa na kikosi kamili cha Tanzania chini ya uongozi wa Mugisha Katura na hapo nyuma kabla ya uongozi wake.
Wakongwe watakosa huduma ya kiungo mwenye mabavu Mugisha anae uguza majeraha yake, huku katibu wa sasa Mbarouk akitarajiwa kuongoza timu hiyo ya wakongwe akishirikiana vyema na Husein Kiza, Mbonde, Japhari Kisiwani.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.