vilabu

Kukipiga tutakipiga, gharama ya safari atuko teyari

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imesema wako tayari kucheza na mabingwa wa Carling Cup, Birmingham City ya England, lakini hawako tayari kulipa tsh bilioni moja kugharamia ujio huo unaoratibiwa na kampuni ya Legal Sports.
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, akizungumza na waandishi wa habari, alisema gharama ya safari ya Birmingham ambayo ni dola mil 1.8 za marekani, zinatakiwa kubebwa na klabu za Simba na Yanga ambayo ni kujiingiza kwenye matatizo. “Awali kabla ya Rage kutangaza kuileta timu hiyo, alinipa nyaraka za kuombea fedha katika mojawapo ya makampuni ya Uingereza, ili kufanikisha kucheza na timu mojawapo kutoka huko, lakini nilikataa baada ya kutambua kwamba atakayehusika na mpangilio huo ni mmoja wa watu wasio wema katika maendeleo ya jamii na kumtaka Rage amuondoe mtu huyo,” alisema Nchunga.
Nchunga aliendelea kufafanua kuwa Rage hakumaliza taratibu za makubaliano na badala yake alimuaga kwamba anakwenda Marekani, halafu atapitia Uingereza kwa ajili ya mazungumzo na Birmingham, ambako alirudi na nyaraka ambazo zilikuwa hazina jina la mtualimuomba amuondoe, ingawa katika nyaraka nyingine jina la huyo mtu lilikuwemo.
Nchunga aliongeza kwa kusema, uwanja wa taifa mapato ya juu yalikuwa mil 600 katika mechi ya kwanza ya mashindano kati ya Tanzania ‘ Taifa Stars’ na Msumbiji wakati Birmingham hawana majina makubwa ya kusukuma mashabiki kufulika.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.