"Makocha wa stars kutoka nchi moja hivi maana yake falsafa zao zinafanana! hivi ni kweli makocha wote wakitanzania wanafanana falsafa au wanafanana lugha.....napata shaka kidogo na usemi huu. Nahisi tunajipotosha wenyewe." kauli ya mdau kwa mchambulizi mashuhuri nchini Shafih K Dauda.
Tff walimtangaza kocha Kim Poulsen kutoka Denmark, kuwa kocha wa timu za vijana huku kichecheo kikubwa kikiwekwa ni kutokana na kufanana falsafa kwa kuwa wanatoka nchi moja.
Mnaweza kuwa mmetoka katika familia moja na kutofautiana katika falsafa kwa kiasi kikubwa na hivyo kutokuwa ajabu watu wanchi moja kupingana katika falsafa ya mpira.
Tunafahamu wa Denmark wanapenda mpira wa kujihami mno ndo maana ckushangaa kwa baadhi ya mechi za Stars chini ya Poulsen kucheza bila ya mshambuliaji, hii si maana kuwa kila kocha kutoka Denmark wana aina hiyo ya mchezo.
Tukienda Brazili, wa Brazil na makocha wengi wa kibrazil hawapendi kucheza mchezo wa kujihami, falsafa yao ni kushambulia, lakini ndani ya Brazil kumeibuka makocha wenye falsafa ya kujiami kwanza kama Maximo, Dunga na wengineo, hivyo hivyo ukienda Ureno, Hispania, Uingeleza, Italia, Ufaransa, na nchi nyinginezo hata kwa majirani zetu Kenya makocha wao wanatofautiana katika falsafa ya mpira.
Kutoka nchi moja si kigezo cha kufanana falsafa, tunaona falsafa ya Kihwelo, Marsh, Minziro, Mwaisabula, japo kuwa ni watanzania lakini falsafa zao zinatofautiana.
Kama uteuzi wa kocha wa timu za vijana, kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen alishirikishwa ndipo suala la falsafa yaweza kuingia hapo, kwani Jan anaweza kuwa anamtambua Kim vizuri kuliko Tff wanavyo mtambua.
Kutoka katika nchi moja si kigezo cha kufanana katika falsafa ya kitu husika.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment