wachezaji

Pamoja na kutikisa nyavu bado akubaliki

Mwaka 2007 walimlaumu sana Maximo kwa kumganda mshambuliaji asiye funga mabao, huku wakimzungumza vibaya kiasi kilicho pelekea kupotea katika ramani ya soka ya Tanzani.
Hivi karibuni amekuwa mfumania nyavu kila anavyo teremka uwanjani. Cha ajabu bado mashabiki wanaendelea kumbeza.

Gaudence Mwaikimba ni wachezaji wachache katika ligi kuu ya vodacom wenye umbo kama lake, akiwa ameenda hewani mwili umejaa, kiac kwamba kocha yoyote amuonapo kabla ajagusa mpira angependa kuwa naye.
Mwaikimba alitambulishwa katika soka la bongo kwa mara ya kwanza na timu ya wauza mitumba wa Ilala, Ashanti United, ambayo imetutambulishie nyota wengine wengi kama Juma Jabu, Adam Kingwande, Jabir Azizi, Redondo na wengineo wengi.

Nguvu aliyo kuwa nayo, ufumaniaji nyavu wakati akiwa Ashanti ulipelekea uongozi wa yanga umsajili mwaka 2006, huku akipata nafasi ya kuichezea timu ya taifa.
Akiwa yanga alishindwa kungara huku akijikuta akizomewa kila aingiapo uwanjani na hatimaye akawa mchezaji wa kukaa kwenye benchi ama kwenye jukwaa.

Alipoteza kujiamini na kupelekea kutemwa kwenye timu ya Taifa, na pale alipo pata nafasi katika kikosi cha yanga alishindwa kuperform, kutokana na presha ya mashabiki.

Katika msimu wa 2009/2010 alijiunga na Prisons ya Mbeya baada ya kurushiwa virago yanga. Katika mwaka huo Mwaikimba aliwashangaza wengi pale ilipo ripotiwa anaenda Vitenam kufanya majaribio lakini alishindwa kufanya majaribio baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za safari.
Kuustajabu kwa umma wa kitanzania kutokana na performance yake kuwa chini na inasemekana aliye msukia safari alikuwa ni Danny Mrwanda.

Baada ya kushindwa kufanya majaribio alirejea kwenye ligi kuu huku na kushindwa kuisaidia timu ya Prisons kusalia ligi kuu na hivyo kushuka daraja wakati yeye akipata ulaji katika klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera.

Mwaikimba ndani ya msimu wake wa kwanza akiwa na wakatamiwa wa Kagera aliweza kutikisa nyavu mara 13 katika mechi 20 alizocheza, akiwa nyuma kwa magoli mawili ya mfungaji bora wa msimu Mrisho Ngassa huku akiwa bwaga kina Jerry Tegete, Mgosi, Mwape na Samatta waliocheza nusu msimu. Kitendo hicho kilimpelekea kocha wa Taifa stars Poulsen kumwita katika mashindano ya CECAFA pamoja na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya japo kuwa alishindwa kungara na kupelekea kutemwa baada ya mashindano kwisha.

Mwaikimba akiwa na timu ya Mbeya aliendelea kuudhihirishia umma kuwa bado yumo kwenye chati baada ya kuibuka mfungaji bora katika kombe la kili taifa baada ya kutikisa nyavu mara 8 katika mechi 6 alizocheza, huku Jerry Tegete akichemka kumfukuza na kuisaidia mbeya kutwa kombe.

Mwaikimba bado anakazi ya kuwadhihirishia umma kuwa yeye ni bora katika ligi kuu msimu ujao kwa kuendeleza wimbi la kufumania nyavu. Mwaikimba ni yule aliye kuwa Ashante akaenda yanga kisha Prisons na sasa Kagera tofauti ni kwamba hachezi na presha za mashabiki vile vile karejesha kujiamini

Mshambuliaji bora ni yule anayetupia


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.