Pesa ndio zinazo zungumza baada ya pendekezo la kocha juu ya wachezaji anao wataka. Hiyo kauli inakaa baada ya uongozi wa klabu ya Simba kutangaza wanaweza kusajili mchezaji toka klabu yoyote ile ambaye kocha, Moses Basena akimuhitaji kufanya naye kazi hata kama yuko yanga.
Katika siku za karibuni Simba walihusishwa juu ya usajili wa Kenneth Asamoah ambaye yuko mbioni kukamilisha taratibu za kujiunga na yanga, na majuzi kulíibuka fununu la Simba kutaka kumsajili beki wa Taifa stars na Yanga Nadir Haroub Canavaro. Vitendo hivyo viliinua hasira kwa uongozi wa Yanga.
Kauli hiyo inaweza ikazidi kuchochea hasira kwa yanga na kuwa weka wachezaji wake chini ya ulinzi mkali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa simba iko vizuri kifedha na hivyo kupelekea suala la usajili kuwa mrahisi, na watanyakuwa mchezaji yoyote toka ndani au nnje ya nchi ambaye kocha amempendekeza kutoa msimbazi. "Unajua unapozungumzia usajili ujue pembeni yake unaongelea pesa ambayo kwa sasa si tatizo kwetu Simba hivyo tutachukulia kwa umakini mkubwa mapendekezo ya mwalimu, hii nina maana hata kama ni wa Yanga ama klabu nyingine ya ndani au nje ya nchi lakini hilo litafanyika kwa kuzingatia utaratibu," alisema Kaburu.
Katika hatua nyingine Kaburu alisema kuwa usajili wao utaendelea kufanywa kwa usiri hadi pale muda muafaka uliowekwa na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) utakapo wadia.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment