Kili Taifa cup 2011 iliendelea leo kwa michezo miwili ya robo fainali, iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Michezo hiyo miwili umeshuhudia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 na timu ya mkoa wa Ruvuma wakifungishwa vilago baada ya kukubali kufungwa.
Mchezo wa kwanza uliwakutanisha Mbeya na Ruvuma na kushuhudia Mbeya ikitinga nusu fainali kwa ushindi wa goli 3 kwa 2.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na huku mashabiki wakiendelea kushuhudia makali ya Gaudence Mwaikimba aliyo anza nayo katika ligi kuu akiwa na uzi wa Kagera Sugar, baada ya leo kuifungia Mbeya magoli mawili.
Mchezo wa pili ulimnyamazisha kocha mwenye maneno Jamhuri Kihwelu 'Julio' baada ya kushindwa kulitwa kombe la kili taifa cup kwa mara ya pili mfululizo. Julio alitamba misimu miwili mfululizo ya kili taifa cup alipokuwa anakiongoza kikosi cha Ilala kabla ya mwaka jana kufungwa na kushindwa kulitetea kombe ambalo lilichukuliwa na Singida iliyokuwa inaongozwa na Suleiman Matola.
Julio mwaka huu aliingia katika mashindano haya na kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 ambayo imefungwa na timu ya mkoa wa Kagera kwa mikwaju ya penati.
Kagera na timu ya taifa chini ya miaka 23 walimaliza dakika 90 wakiwa wamefungana magoli 2 kwa 2 na hapo mikwaju ya penati ikachukua hatua.
Kagera iliibuka kidedea kwa kuzamisha mikwaju 3-1.
Kutokana na matokeo ya leo nusu fainali ya pili itakayochezwa mei 25 itawakutanisha Mbeya na Kagera.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment