vilabu

Simba waomba muongozo CAF

Baada ya simba sc kushinda rufaa yake dhidi ya TP Mazembe, wametuma barua Caf kutaka kufahamu kama wanaweza kuwa tumia wachezaji Samatta na Ochan katika mchezo wa Wydad ya Morocco utakao pigwa kati ya tarehe 27, 28, 29 mei mwaka huu.
Simba wamewauza wachezaji Mbwana Samatta na Patrick Ochan kwa mabingwa mara mbili Africa TP Mazembe, wakati dirisha la usajili wa klabu bingwa na kombe la shirikisho Africa bado alijafunguliwa rasmi.
Katika hatua nyingine simba wamesema watatumia michuano ya Kagame kujaza nafasi za wachezaji kutoka nnje ya nchi zilizo salia.

MGOSI ANGOJA BARUA.
Mussa Hassan Mgosi amesema hawezi kuhudhuria mazoezi ya simba kwa kuwa alisimamishwa kwa tuhuma za kuhujumu timu.
Mgosi ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakuenekana katika mazoezi ya simba yaliyoanza jana kujianda na Wydada, huku Mbwana Samatta akiwa amerudi Congo kujiunga na TP Mazembe. Wakati Emanuel Okwi akitarajiwa kujiunga na timu leo.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.