vilabu

Simba wapewa kibarua

Timu ya simba wanajikuta katika wakati mgumu baada ya kupewa nafasi katika ligi ya klabu bingwa Afrika baada ya Mabingwa watetetezi TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuondolewa katika michuano hiyo.
Huamuzi huo umefuatia baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika Caf kupitia pingamizi la Simba juu ya mchezaji Janvier Besala Bokungu, ambaye alichezeshwa katika pambano la Mazembe na Simba wakati akiwa ajakamilisha taratibu za uwamisho.
Shirikisho la Soka Afrika CAF baada ya kupitia pingamizi hilo wamefikia uwamuzi wa kuivua Ubingwa Mazambe na hivyo Simba kupata nafasi ya kucheza na timu ambayo ilifungwa na Mazembe katika hatua ya mtoano, Wydad Casablanca ya Morocco katika uwanja ambao utatangazo hapo baadae.
Endapo Simba wakiwafunga waarabu hao watatinga katika hatua ya nane bora ambayo waliifikia mwaka 2003 baada ya kuitoa Zamaleki.
Simba ambayo ilishaanza kufunja timu kwa kuwauza baadhi ya nyota watakuwa na kibarua kigumu cha kuwakosanya nyota wake waliosalia kwa ajili ya pambano hilo litakalo chezwa katika uwanja utakao tangazwa wiki ijayo.

aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.