UONGOZI wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam unatarajiwa kutoa maamuzi mazito kuhusu viongozi na wachezaji walioihujumu timu hiyo na kushindwa kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tamko hilo, lilitolewa wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambao ulijadili masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya Simba. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, hatua hiyo inakwenda na uamuzi aliofikia wa kuahirisha safari yake nchini Uturuki kwa ajili ya kufuatilia mikakati ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu klabu hiyo, kutokana na Simba kurejeshwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rage alitumia fursa hiyo, kuwaomba wanachama waliohudhuria mkutano huo uwape ridhaa ya kuwaadhibu waliofanya makosa hayo.
Mbali ya Rage, pia Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mganda Moses Basena, ameahirisha programu yake ya timu ya taifa ya nchi hiyo, The Cranes, na kuwasili nchini juzi, kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo ambayo yanatarajiwa kuanza leo jioni baada ya wachezaji wote kuwasili, naye ameahirisha.
Aidha Rage alisema, Simba inaendelea kujipanga kwa ajili ya maendeleo, ikiwemo kupandisha vijana wanane kutoka timu ya vijana inayonolewa na King Abdallah Kibadeni, kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
Pia Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, wanakusudia kumpeleka masomoni kocha huyo Ulaya, kwa ajili ya kuongeza ujuzi zaidi ili aisadie Simba, huku mpango mwingine ukiwa ni kuanzisha timu ya vijana chini ya miaka 14. Alisema, ili kufanikisha maendeleo ya soka la Simba, wanajipanga kuwatumia makocha ambao walikuwa wachezaji wa timu hiyo ambao ni pamoja na Seleman Matola, Saidi Swedi na Amri Saidi.
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, Rage alitumia mkutano huo kama jukwaa la siasa na kutia kibwagizo cha ‘CCM Oyee’, badala ya ‘Simba Oyee’ jambo ambalo lilizua minong’ono miongoni mwa wanachama.
Katika hatua nyingine, klabu hiyo inajipanga kutumia sh 250 ,000 ,000 kwa usajili wa msimu wa 2011 /12 unaotarajia kuanza Juni mosi. Hatua ya kutumia fedha hizo, imekuja baada ya kukusanya mapato ya sh 678 ,356 ,487 na kutumia sh milioni 666 ,238 ,568 na kubaki na sh 12 ,117 ,919 katika benki za NMB na CRDB ikiwa ni mwaka mmoja wa uongozi wa Mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Kwa mujibu wa Mkaguzi kutoka kampuni ya Audit International Venance Kusare mapato yalitokana na makusanyo ya milangoni sh 153 ,313 ,677 , wadhamini sh 288 , 240 ,000 , zawadi sh 45 ,000 ,000 , bidhaa sh 29 ,000 ,000 , michango na wahisani sh 136 ,300 ,000 , ada za mwaka za wanachama sh 61 , 000 na mkopo sh 25 ,516 ,762. Kusare aliweka bayana matumizi ni mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi sh 243 ,150 ,000 , posho kwa benchi la ufundi na wachezaji sh 42 ,377 ,000 , malazi na chakula sh 74 ,873 ,700 , gharama za usafiri sh 24 ,332 ,000 , vifaa vya michezo sh 60 ,000 ,000 , gharama za usajili wa wachezaji sh 195 ,200 , 000 , ukarabati wa majengo sh 11 ,873 , 100 na vifaa vya ofisi na gharama nyingine ni sh 14 , 432 ,768.
Aidha, mkutano huo mkuu, ulipitisha wadhamini wanne ambao ni Abdul Wahab, Ramesh Patel, Hamis Kilomoni na Ally Sykes.
source: freemedia.co.tz/daima

0 comments:
Post a Comment