wachezaji

Ulimwengu kutua leo kuwakabili Wanigeria

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania pamoja na kituo cha AFC cha nchini Sweden, Thomas Ulimwengu anatarajiwa kuwasili leo akitokea nchini Ujerumani.

Ulimwengu ambaya alifanya majaribio katika klabu ya TP Mazembe na kufuzu alipata mwaliko nchini Ujerumani kwa ajili ya majaribio katika klabu Hamburg SV ambapo bado anaendelea na majaribio.
Ulimwengu anarejea nchini kuwakabili timu ya vijana ya Nigeria katika harakati ya kusaka nafasi ya kushiriki Olympic mwakani jijini London Uingeleza, mchezo utakao chezwa saa moja usiku katika uwanja wa Taifa hapo juni 5.

Kwa upande mwingine, Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah amewaomba wadau wajitokeze kuichangia timu ya Taifa ya Vijana inayo kabiliwa na ukata.
Timu hiyo iko kambini kujianda na mchezo wa juni 5 dhidi ya Nigeria.
aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.