wachezaji

Wakati Ngassa arudi yanga, Okwi atimkia Kaizar chief

aamsuni:

Wachezaji mahiri wa timu za taifa za vijana chini ya miaka 23 pamoja na wakubwa katika ukanda wa Afrika mashariki, Mrisho Ngassa (Tanzania) na Emanuel Okwi (Uganda) wako katika njia tofauti ya kuziama klabu zao.
Ngassa ambaye alinukuliwa na baadhi ya waandishi wa habari na wachambuzi wa mpira wa mguu nchini anataka kurejea yanga kwa kukwepa majungu ya mashabiki pale Azam.
Pamoja na yanga kuandika barua kwa Azam fc ya kumtaka mshambuliaji huyo mwenye kasi uwanjani, uwongozi wa Azam umesema hauzwi kwa dau lolote lile ndani ya nchi.
Wakati Ngassa akisaka namna ya kurudi Jangwani ni mambo tofauti kwa Mganda anaetamba na uzi mwekundu na mweupe ambaye alisajiliwa akitokea SC Villa ya Uganda. Okwi sasa anangoja viza ya kwenda Afrika kusini kwa ajili ya majaribio katika klabu ya Kaizar Chiefs inayoshiriki ligi kuu ya Afrika kusini.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.