Mchangani

Watoto wa mjini uso kwa uso na watoto wa jiji

Watoto wa mjini toka Dar es salaam, timu ya mkoa wa Ilala watakutana na watoto wa jiji la miamba (rock city), timu ya mkoa wa Mwanza katika nusu fainali ya kwanza ya kili taifa cup 2011.
Mpambano huo utaanza saa kumi alasiri katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Ilala ambayo inaonekana kuimalika kadri wanavyozidi kuteremka uwanjani, wametinga hatua hiyo baada ya kuichalaza Singida magoli matatu bila majibu baada ya kuibuka kidedea katika kituo cha Morogoro.
Mwanza ambayo inamtegemea Jerry Tegete wa yanga kuongoza mashambulizi katika kuingamiza timu ya Ilala. Mwanza wametinga hatua hii baada ya kuichalaza Arusha magoli mawili kwa moja baada ya kuibuka kinara wa kituo cha Mwanza.

Bingwa wa Michuano hii ya Kili taifa cup atanyakuwa kitita cha Sh.milioni 40 , mshindi wa pili Sh.milioni 20 wakati wa tatu sh.milioni 10.

aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.