Uongozi wa yanga umeijia juu timu ya simba kwa kitendo cha kufuata nyayo zao na kuongea na wachezaji wao kinyume na taratibu. Hiyo kauli imefuati baada ya tetesi kushamiri mtaani kuwa simba wako mbioni kumnasa beki mahiri nchini hivi sasa Nadir Haroub 'Canavaro' kwa kitita cha Tsh mil 50.
Ofisa habari wa yanga, Luis Sendeu alisema kuwa wako katika harakati ya kumtafuta kiongozi wa Simba anayefanya mazungumzo na wachezaji wenye mikataba ya kuitumikia klabu ya yanga, na watamshtaki katika kamati ya nidhamu ya Tff.
Simba waliingia katika njia ya yanga katika harakati ya kumsajili mshambuliaji toka Ghana Kenneth Asamoah, na hapo majuzi kukaibuka tetesi ya kumsajili Canavaro mwenye mkataba wa miaka miwili kuitumikia yanga.
“Sisi tunashangaa kwa kuwa kila mara Simba inatuingilia kwa wachezaji wetu na kadhalika simnakumbuka ya Asamoh (Keneth) ilivyokuwa, sasa sisitukiamua kujibu mapigo kwa kuwafuatia wachezaji wao isijeikawa ndio kuibuka kwa matatizo,” alitabanaisha Sendeu mbele ya waandishi wa habari.
Aliongeza kuwa “ni kwamba huyu kiongozi wa Simba aliyekuwa akitaka kumsainisha Canavaro kihunihuni sisi tutahakikisha kuwa tunamfikisha katika kamati ya nidhamu ya TFF iliashughulikiwe kikamilifu na haya ni mambo ya kizamani tu,”alisema Sendeu.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment