VPL

ASAMOAH AFUNGUKA, YANGA WAWASAMBARATISHA WAGOSI

Mshambuliaji wakimataifa toka Ghana anaekipiga kwa mabingwa wa Tanzania Bara Yanga, Kenneth Asamoah leo kafunguka kwenye michuano ya ligi kuu ya Vodacom "VPL" pale Yanga walipo wakaribisha Coastal union.

Mashabiki wa yanga wametoka nafuraha kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Taifa tangu wafungue msimu huu wa 2011/12 katika mchezo dhidi ya Simba. Yanga hii leo wameichapa goli 5 wagosi wakaya.

Sherehe ya magoli yalifunguliwa na Kenneth Asamoah kabla ya mchezaji anae rudi katika kiwango chake tangu atoke katika majera ya mda mrefu Shamte Ally kufunga la pili.

Davis Mwape alifunga goli la 3 katika dakika ya 22 kabla ya Nurdin Bakari kufunga goli la 4 katika dakika ya 41. Timu hizo zilikwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa magoli manne bila.

Alikuwa Mghana Kenneth Asamoah kuhitimisha kalamu ya mabao baada ya kufunga goli 5 kwa yanga likiwa la pili kwake katika mchezo huo ambao ulikwisha kwa yanga kuibuka na usindi wa 5-0.

Yanga kabla ya mchezo huo walikuwa hawajashinda mchezo wowote msimu huu katika uwanja wa Taifa baada ya kufungua msimu kwa kufungwa na Simba katika mchezo wa ngao ya jamii, ukifuatia nasare dhidi ya Rufu shooting kabla ya kufungwa na Azam fc.


MSIMAMO WA VPL. Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (8) 18
2. Azam FC (8) 15
3. JKT Oljoro (8) 13
4. Mtibwa Sugar (8) 12
5. JKT Ruvu (8) 12
6. Yanga (8) 12
7. Ruvu Shooting (8) 11
8. Toto Africa (8) 9
9. Moro United (8) 9
10. Africa lyon (8) 9
11. Kagera Sugar (8) 8
12. Polisi Dodoma (8) 7
13. Villa Squad (8) 5
14. Coastal Union (8) 4

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.