simba

KERR: MAGANGA NA KIMWAGA WATAIBEBA SIMBA SC

Mshambuliaji wa Simba Joseph Kimwaga 
Kocha wa timu ya Simba, Dylan Kerr, ametamba kuwa kikosi chake kina uwezo wa kuibuka na ushindi katika mechi ijayo ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City bila kuwapo kwa mshambuliaji wao kinara, Mganda, Hamis Kiiza ambaye ni majeruhi.

Mbeya City itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ifikapo Oktoba 17 mwaka huu na baada ya siku tatu, Wekundu hao wa Msimbazi watakabiliana na Prisons kwenye uwanja huo huo.

Kerr alisema hakukiandaa kikosi chake kwa kumtegemea mchezaji mmoja na kukosekana kwa Kiiza haitokuwa sababu ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo hiyo miwili ya ugenini.

“ Timu inawachezaji zaidi ya 20, siwezi kumtegemea mchezaji mmoja, tutacheza michezo yetu ya ugenini kwa lengo la ushindi na kukosekana kwa Kiiza haitakuwa sababu ya sisi kupoteza pointi,” alisema Kerr.

Kocha huyo aliongeza kwamba tayari ameacha kumuandaa mshambuliaji mwingine chipukizi, Boniface Maganga, kwa ajili ya kurithi mikoba ya Kiiza huku akifurahishwa na maendeleo ya Joseph Kimwaga.

Aliongeza kwamba wachezaji hao walionyesha juhudi katika mechi iliyopita dhidi ya Stand United ambayo walipata ushindi wa bao 1-0.

“Kiiza hatacheza mechi hiyo, ila wapo wachezaji wengine ambao tumewaandaa na mmoja wao ni Boniface, siku si nyingi atakuwa mmoja wa washambuliaji wakali kwenye Ligi ya Tanzania,” alisema Dylan

CHANZO: NIPASHE

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.