Azam FC wamekanusha taarifa ya kuwa wako katika mikakati ya kuwatimuwa Simba na Yanga katika uwanja wake uliopo Chamanzi.
Jana mtandao huu zilinasa taarifa za uongozi wa Azam ziko mbioni kuzitimua Simba na Yanga katika uwanja huo kwa kuwa Simba na Yanga zinamashabiki wengi ambapo uwanja una uwezo wa kuchukuwa wa chache. Taarifa hiyo ilijitokeza katika vyombo vingine mbalimbali.
Katibu wa Azam FC bwana Idrissa Nassoro alisema kuwa Azam hawawezi kuzuiya timu yoyote kucheza mechi zake katika uwanja huo kwa kuwa umejengwa ili utumike.
TIMBE ABAKIZA 2.
Kocha mkuu wa Yanga Sam Timbe alipewa michezo mitatu kuhakikisha kikosi hicho cha Jangwani kinabadilika baada ya kufungwa na Azam FC jumapili iliyopita katika uwanja wa Taifa.
Mchezo wa jana dhidi ya villa squad ilikuwa ni miongoni mwa hiyo michezo mitatu ambapo alishinda goli 3-2 na hivyo kubakisha michezo miwili ambapo jumapili hii watawakaribisha majeruhi Coastal union katika dimba la Taifa.
0 comments:
Post a Comment