CAF

CAF YAINGIA MKATABA WA KURUSHA MATANGAZO

Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF, limeingia mkataba wa kurusha matangazo ya mechi za kufuzu kombe la Dunia mwaka 2014 yatakayo fanyika nchini Brazil na makapuni B4 toka Italia na Lagardere Sport toka Ufaransa pamoja na Sportfive.

Kitendo hiko kimetokana na makubaliano yaliyofikiwa hapo mei 31 mwaka huu na vyama vya soka vya nchi husika zilizoko chini ya CAF na hivyo CAF kuingia mkataba na hayo makampuni kwa kuwapa haki za kurusha matangazo hayo.

Raisi wa CAF Mr Issa Hayatou alisigni kwa niaba ya Shirikisho wakati Mr Bianchi na Mr Le Marchand walisigni kwaniaba ya B4 na Lagardère Sport wakati washerehe iliyofanyika makao makuu ya CAF Cairo, Egypt.

Mechi za kufuzu kwa ukanda wa Afrika zitaanza November mwaka huu (2011) mpaka November 2013 na itahusisha mataifa 52.

Mkataba unausisha haki za matangazo ya TV na masoko katika michezo yote ya Kufuzu kuelekea Brazil kushiliki kombe la Dunia mwaka 2014. Mabango yasiyopungua kumi (minimum of tena) ya matangazo yataachwa kwa mashirikisho mwanachama.

Chama mwenyeji na channel ya timu mwenyeji atapewa kibali cha kurusha matangazo bila gharama yoyote ile (the Host Federation and the Host Broadcaster will be entitled to broadcast each Home Match live, free to air by terrestrial means only).


Raisi wa CAF alisema moja ya malengo ya mkataba huu ni kuzipatia nafasi "less privileged countries" kuonekana mechi zake kimataifa katika kiwango kilicho bora

Mr Hayatou aliongeza pia makubaliano hayo yatawezesha mashirikisho kuongeza mapato yao huku taratibu za kugawanywa hizo pesa zitapangwa katika kikao kitakacho September 28 mwaka huu, huku kiwango cha chini shirikisho kupokea inatazamiwa kuwa dollar za kimarekani millioni 23.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.