VPL

GUMBO AIANZISHA LIGI YANGA, KUPANDA MPAKA NAFASI YA 6

Yanga wameanza ligi ndio kauli inayowezwa kusemwa na mashabiki wa timu hiyo ya mitaa ya Jangwani kufuatia goli la kiungo Rashid Gumbo zidi ya timu yake ya zamani African lyon.

Leo katika uwanja wa Azam Yanga walikaribishwa na wanambagala African lyon katika mchezo uliokwisha kwa ushindi wa kwanza kwa yanga ndani ya miezi 2 wa goli 2-1.

Yanga walikuwa wa kwanza kuzishuhudia nyavu za African Lyon kupitia kwa Davis Mwape mnamo dakika ya 36, kabla ya Hamisi Shengo kuisawazishia Lyon goli katika dakika ya 43.

African lyon na Yanga walikwenda mapumziko wakiwa sare ya goli moja kwa moja. Na katika dakika ya 63 alikuwa kiungo aliyetamba na timu za Mtibwa Sugar, African Lyon, Simba kabla hajatua yanga msimu huu Rashidi Gumbo kuifungia Yanga goli muhimu katika mchezo wa leo.

Mpaka mwisho wa mchezo Yanga 2-1 African lyon na hivyo yanga kujinasua toka mkiani mpaka kushika nafasi ya 6.


MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (5) 13
2. JKT Ruvu (5) 9
3. Mtibwa Sugar (5) 8
4. Moro United (5) 8
5. Azam FC (5) 8
6. Toto Africa (5) 7
7. Yanga (5) 6
8. JKT Oljoro (5) 6
9. Africa lyon (5) 5
10. Coastal Union (5) 4
11. Villa Squad (5) 4
12. Kagera Sugar (5) 4
13. Ruvu Shooting (5) 4
14. Polisi Dodoma (5) 3

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.