Beki toka Uganda aliyetamba na Simba katika rekodi ya timu hiyo kucheza bila kufungwa msimu wa 2009/10, Joseph Owino Gere amemwaga wino wa kuitumikia Azam FC.
Owino alipata majeraha yaliyo muweka nnje takribani msimu mzima uliokwisha na kupelekea kuachwa katika usajili wa Simba anatarajiwa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Kusaini kwa Owino kunamaanisha mchezaji mmoja wa kigeni katika kikosi cha Azam FC hataondolewa katika usajili wa dirisha dogo kumpatia nafasi Owino kucheza, kwani ligi ya msimu huu unaruhusu wageni wa 5. Azam ina wachezaji watano wa kigeni ambao ni Kipre Tchetche (Ivory coast), Nafiw na Wahab (Ghana), Obrein (Serbia) na Kapteni Ibrahim Shikanda (Kenya).
Inasemekana kuwa Azam FC waligharamikia matibabu ya beki huyo anayesifika kuanzisha mashambulizi na kuwatuliza wenzake wakati timu ikiwa kwenye presha.

0 comments:
Post a Comment