VPL

Kivumbi kuwaka Taifa na Kaitaba

Kivumbi cha ligi kuu ya Tanzania Bara 'VPL' kinaendelea leo katika viwanja vya Kaitaba na Taifa kwa kuwakutanisha Azam na Yanga pamoja na Simba na Kagera Sugar.

SIMBA Vs KAGERA SUGAR.

Uwanja wa Kaitaba ni katika viwanja ambavyo ni nadra mgeni kutoka na ushindi na hivi leo Kagera Sugar watawakaribisha timu ambayo haijapoteza mchezo na kuruhusu nyavu za kuguswa Simba.

Simba wamecheza michezo mitano wametoa sare mmoja na kusinda 4 huku wakiwa hawaja fungwa goli hata moja. Leo watakuwa wanadhamira ya kuendeza rekodi yao watakapo wavaa timu hiyo ngumu.

Kagera Sugar mambo bado hayajamkalia sawa msimu huu baada ya kutoa sare 4 na kufungwa mchezo mmoja na leo wanatazamia rekodi ya uwanja wao wa Kaitaba kuwabeba. Kaitaba panasifika kama sehemu ya kutibuliya rekodi za timu zinazoshuka hapo zikiwa hazijafungwa.

Simba leo watakuwa kamili baada ya urejeo wa Emanuel Okwi aliyekuwa Maputo na timu yake ya Taifa ya Uganda pamoja na Felix Sunzu aliyekuwa anatumikia adhabu yake.


AZAM FC Vs YANGA.

Azam na Yanga kila mmoja baada ya kushinda michezo yao ya mwisho walijinadi kuanza ligi rasmi baada ya kufululiza sare na timu hizo zinakutana leo katika uwanja wa Taifa.

Yanga watakuwa na kibarua kigumu kuikabili Azam hii leo ambapo Azam wanaonekana kuwa kamili hivi sasa huku kukichangiwa na urejeo na kiuongo anae kuja juu kwa sasa nchini Salum Abubakar 'Sure Boy'.

Hamisi Kiiza ni miongoni mwa wachezaji wanaotazamiwa kuwapa mafanikiwa Yanga na kurejee kwake kunaiongezea nguvu Yanga ambayo itamkosa Haruna Niyonzima na Jerry Tegete hii leo.


EPL.
Mechi kali leo azipo katika ligi kuu ya Bongo tu, bali hata uingeleza leo kunamipambano miwili mikali inatakayo vuta hisia za mashabiki kote duniani.

Michezo hiyo ni:

MAN UNITED Vs CHELSEA

TOTTENHAM Vs LIVERPOOL

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.