VPL

Lamba lamba kumfukuzia Mnyama?

Mechi za ligi kuu ya vodacoma inaendelea leo kwa michezo mitatu katika mikoa mitatu, ambapo Azam FC (Lamba lamba) watakuwa wakisaka mbini za kumfukuzia Mnyama Simba.

MABATINI, Mlandizi Pwani.

Azam FC watakuwa wageni wa Ruvu shooting katika uwanja wa Mabatini, mchezo huo uliyo muhimu kwa kila timu.

Azam FC itashuka uwanjani bila ya baadhi ya nyota wake waliyomajiruhi, akiwemo mshambuliaji toka Ivory Coast Kipre Tchetche, Mserbia Obrein, AbdulHalim.

Pamoja na kukosekana na nyota hao Azam FC bado inao nyota wengine lukuki ambao wanaweza kuwa sababu ya kutoka na ushindi hii leo na kuendelea kumfukuza Simba katika mbio za ubingwa.

Baada ya kushinda michezo miwili mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani Ruvu Shooting hawatakuwa wepesi kuruhusu kufungwa na kupoteza point hii leo.

MICHEZO MINGINE YA LEO.

JKT RUVU Vs VILLA SQUAD katika uwanja wa Azam

TOTO AFRICAN Vs JKT OLJORO, katika uwanja wa CCM Kirumba

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.