Kijana toka visiwani Zanzibar anaekipiga Chelsea Adam Nditi inasemekana teyari ashachukua urai wa Uingeleza hivyo kumnyima nafasi ya kuitumikia Taifa Stars kwa kuwa Tanzania wana uraia wa nchi moja.
Kitaa cha Aboodmsuni ambako kilipotea kwa mda kilitembelea mtaa wa jarida la mpira wa miguu Namba 10. Na kukutana na taarifa kuhusu bwana mdogo huyo Nditti.
Twende Kitaani:
Nditi aliyeanza kwenye chuo cha kukuza vipaji cha klabu hiyo amekuwa mchezaji wa kutumainiwa katika kikosi cha vijana cha umri wa miaka 18 kwa zaidi ya misimu mitatu sasa.
Nditi ambaye amekuwa chini ya kocha Muingereza Neil Bath katika timu ya chuo, sasa baada ya kupabndishwa timu ya vijana, atakuwa chini ya kocha mwingine Muingereza, Adrian Viveash.
Adam Nditi alizaliwa Septemba 18, mwaka 1994, Kikwajuni Zanzibar kabla ya baadaye kwenda England kujiunga na chuo cha soka cha Chelsea ambako sasa amepanda hadi U-21.
Hata hivyo, kuna wasiwasi kama Nditi anaweza kuichezea Tanzania, kutokana na habari kwamba kijana huyo tayari ana uraia wa Uingereza na serikali ya Tanzania hairuhusu raia wake kuwa na uraia wa pili.
0 comments:
Post a Comment