mtazamo

Ngassa bado yumo

Hivi ni kweli mshambuliaji wa Azam FC, Mrisho Khalfan Ngassa kiwango chake kimeshuka baada ya kutoka Marekani?
Mashabiki wengi wa soka la Bongo wanadai Ngassa kashuka kiwango kama walivyo kuwa wanasema mara tu baada ya kujiunga na Azam FC na kucheza mechi 5 za ligi kuu bila ya kuziona nyavu, wakati alikuwa anashika nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa amefunga magoli 14 nyuma kwa goli moja la Mussa Mgosi katika msimu wake wa mwisho wa ligi akiwa yanga (2009/10).

Lakini Ngassa huyo ndiye aliyeibuka kinara wamabao katika msimu huo wa 2010/11 akifunga magoli 16 huku akianza kuziona nyavu katika mechi ya 6 ya ligi kuu ya vodacom 'vpl'.

Msimu huu kashacheza michezo mitano bila ya kuziona nyavu na isiwe sababu ya kumzomea ama kumsema kiwango kimeshuka. Mchezo unao fuata na Coastal union ni mchezo wake wa 6 ukiwa ni wa 7 kwa timu, bila shaka atakuwa mmoja atakae tikisa nyavu kama Azam FC watashinda mchezo huo.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.